Popular Posts

Friday, 26 June 2015

SOMO: IMANI



Sehemu ya 3.



Namshukuru sana MUNGU baba wa Bwana wetu YESU kristo aliyetupa uzima na afya njema, nakutuwezesha kuiona tena siku ya leo. pia nikushukuru sana wewe ndugu yangu mpendwa kwa kuendelea kujumuika pamoja nasi katika mfululizo wa masomo haya kutoka katika huduma ya Ruhama healing ministry.wiki iliyopita tulimaliza kwa kuweka msisitizo zaidi kaatika kulisoma na kulitendea kazi neno la MUNGU. karibu tuendelee sehemu ya tatu.

AINA TATU ZA NENO.


Tunaposema juu ya kulisikia  na kulitendea kazi neno, tunamaanisha aina tatu za neno, au maeneo matatu ambayo neno la MUNGU hutenda kazi.


1: LOGOS; Ni neno la kiyunani lenye maana ya neno lililoandikwa, au kwa lugha nyingine ni maandiko.Ukweli ni kwamba neno la MUNGU lililoandikwa ndiyo msingi mkuu wa imani.
Hii ni kwa sababu Biblia haikuandikwa kwa mtazamo wa waandishi bali ni kwamba Roho mtakatifu aliwaongoza kuandika yale yote ambayo MUNGU alikuwa amesema nao.  Au tunaweza kusema walivuviwa na Roho mtakatifu kuandika neno la MUNGU. Kwa hiyo hakuna Biblia nyingine itakayoandikwa tena na kuitwa neno la MUNGU.


2: RHEMA. Ni neno la kiyunani lenye maana ya neno lililofunuliwa, Kufunuliwa hapa haina na kupata kitu kipya ambacho hakijawahi kutokea hapana, ni ile hali ya mtu kupata mwanga fulani kwa msaada wa Roho mtakatifu juu ya maana halisi ya kile ambacho MUNGU alimaanisha wakati anatamka maneno hayo,au neno hilo.
Pia inaweza kuwa na maana ya kupata tafsiri halisi juu ya kile kilichoandikwa ndani ya neno la MUNGU kuhusu maisha yako ya sasa au maisha ya mtu mwingine. Ni ukweli wa neno la MUNGU unaowekwa wazi kuhusu maisha yako ya sasa.

3: PROPHETIC WORD: Ni neno la MUNGU linaloletwa kinywani mwa mtu kwa msukumo wa Roho mtakatifu. Neno hili ni tofauti kidogo na neno la kinabii linalotolewa nabii kwa maana ya mtu anayetumika katika ofisi ya kinabii anapokuwa kwenye utendaji wa huduma yake kama nabii. Ni ukiri wa kiimani ambao ni matokeo ya kulijaza neno la MUNGU kwa wingi ndani yako.
Mtu anayelijaza neno laMUNGU kwa wingi kwa maana ya kulisoma na kujifunza, na hasa mtu huyo anpokuwa mwombaji, neno lile halitavumilia kukaa ndani yake, ni lazima litaanza kudai kutoka nje.
Utamkuta mtu huyo akitamka mambo makubwa kwa imani na yanatokea.

Ezekieli 37:4-10. Akaniambia tena, toa unabii juu ya mifupa hii,uiambie enyi mifupa mikavu lisikieni neno la BWANA.Bwana MUNGU aimbia mifupa hii maneno haya,tazama nitatia pumnzi ndani yenu nanyi mtaishi.nami nitatia mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika ngozi, na kutia pumnzi ndani yenu, nanyi mtaishi nanyi mtajua kuwa mimi ndimi BWANA.Basi nikatoa unabii kama nilivyoamriwa, Hata nilpokuwa natoa unabii , palikuwa na mshindo mkuu, natazama tetemeko la nchi,na ile mifupa ikasogeleana mfupa kwa mfupa mwenziwe. Nikatazama kumbe kulikuwa na mishipa juu yake, nyama ikatokea juu yake, ngozi ikafunika juu yake, Lakini haikuwemo pumnzi ndani yake. Ndipo akaniambia, tabiri uutabirie upepo, mwanadamu ukauambie upepo, BWANA MUNGU asema hivi, njoo kutoka pande za pepo nne ,ee pumnzi ukwapuzie hawa waliouawa wapate kuishi. Basi nikatabiri kama alivyoniamuru, pumnzi ikawaingia, wakaishi, wakasimama kwa miguu yao jeshi kubwa mno.

Ingawa muktadha wa habari hii unahusu wana waisraeli na kifo cha kiroho, kuna kitu kingine tunachoweza kujifunza kupitia habari hii. Kitu hicho si kingine ila ni nguvu iliyopo ndani ya ukiri wa neno ambalo MUNGU analitia katika kinywa chako.
Tumeona hapa kwamba MUNGU anamwambia Ezekieli atabiri Ezekieli anatabiri kwa kutamka kila neno ambalo MUNGU analiweka kinywani mwake au kumwamuru, tunaona hapo baada ya Ezekieli kutabibiri mambo makubwa yanatokea.
Mtu aliye na bidii katika kujifunza neno  MUNGU lile neno huwa linahifadhiwa ndani yake, mtu huyu anapokabiliwa na changamoto fulani katika maisha yake, neno huwa lina kawaida ya kuhama kutoka moyoni kuja kinywani, na linapotamkwa kwa upako linakuwa na nguvu ya kubadilisha mazingira yaliyopo na kuwa kama unavyotaka yawe.
Dunia hii na vyote vilivyomo vimeumbwa kwa neno, kwa maana hiyo ni kwamba vina uwezo wa kusikia sauti ya MUNGU kupitia neno na kutii.

Marko 11:23. Amin nawaambia yeyote atakayeuambia mlima huu ng,oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, bali aamini kwamba hayo asemamayo yanatukia, nayo  
yatakuwa yake,
Ndugu yangu mpendwa katika kristo YESU, ni kweli kwamba MUNGU amewaita watu wengi katika huduma ya kinabii,Na ataendelea kufanya hivyo, lakini napenda uje kwamba nabii wa kwanza wamaisha yako ni wewe mwenyewe.
Kuna changamoto nyingine kwenye maisha hazihitaji nabii kutoka mbali aje kuzitatua, Mungu ameweka nguvu yake ya uumbaji ndani yako ili utamke vitu vitokee.

Mithali 18:21. Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi, na wao waupendao watakula matunda yake.
Hali uliyo nayo kwa kiasi kikubwa imechangiwa na yale ambayo umekuwa unatamkia katika maisha yako. Na mara nyingi tumejikuta tunajitamkia mabaya zaidi kuliko tunavyoweza kujitamkia mema. Tubadirike.
ITAENDELEA


No comments:

Post a Comment