Popular Posts

Thursday, 18 June 2015

SOMO; IMANI

Namshukuru sana na MUNGU aliyetupa neema ya kukutana tena katika mfululizo wa masomo haya kutoka katika huduma hii ya Ruhama healing ministry.Nikukaribishe sana katika somo hili ambalo naamini litakuwa ni baraka sana kwako na kwangu pia.

UTANGULIZI.

ANDIKO. EBR 10;30 Biblia inasema. lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani, akisitasita roho yangu haina furaha naye.
Hapa tunaona maandiko yanasema mwenye haki ataishi kwa imani. kwa maana hiyo ni kwamba mwenye haki akiweka imani pembeni hataweza kuishi.
Au niseme kwamba imani ndio mtaji mkubwa wa kumwezesha mwenye haki kuishi hapa duniani.
Mwenye haki ni mtu aliyempokea YESU kuwa BWANA na mwokozi wa maisha yake, na kuishi kwa kufuata maelekezo yake.

Warumi 1:17 Biblia inasema. haki ya MUNGU inadhihirishwa ndani yake{huyo mwenye kuamini}toka imani hadi imani, kama ilivyoandikwa, mwenye haki ataishi kwa imani.
kumbe kinachomfanya mtu kuwa mwenye haki mbele za MUNGU ni imani iliyomo ndani yake na si vinginevyo.
Na si imani iliyomo ndani yake tu bali imani inayokuwa  kutoka kiwango fulani kwenda kwenye kiwango kingine.
Na kwa kadiri viwango vyako vya imani vinavyoendelea kukua na kuongezeka, ndivyo haki yako mbele za MUNGU inavyokua na kuongezeka.
Kuongezeka kwa haki yako mbele za MUNGU kuna harakisha mabadiliko katika maisha yako, ya kiroho na kimwili.
Wagaratia3:11 inasema. Ni dhahiri kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za MUNGU katika sheria, kwa sababu mwenye haki ataishi kwa imani.
Maandiko haya yote yanaongelea kitu kilekile, kwamba mwenye haki ataishi kwa imani hapa tunapata picha moja tu, kwamba imani ndiyo injini ya kuyasukuma maisha yake na kuyafanya yasonge mbele.
Kwa maana iliyowazi zaidi ya maandiko hayo ni kwamba kama huna imani unapoteza haki yako ya kupokea chochote kutoka kwa MUNGU.
Waebrania 11:6 lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza,kwa maana mtu amwendeaye MUNGU lazima aamini kwamba yeye yuko, na huwapa thawabu wamtafutao.
Hapa inaendelea kutafsiri kwa undani zaidi, kwamba pasipo imani haiwezekani kumpendeza MUNGU, rugha nyepesi ya neno hili ni kwamba kutokuwa na imani ni dhambi.
 Unaweza kuona ni kwa jinsi gani imani ni mhimu katika maisha ya mtu aliyeokoka,  hata wale watakaoenda jehanamu, hawataenda kwa sababu wametenda dhambi sana, ila wataenda jehanamu kwa sababu ya dhambi kubwa kupita zote, nayo ni kukata kumwamini YESU.
kama kuna mtu unafuatilia mafundisho haya na unajua kuwa hujaokoka, huu ndio wakati mwafaka wa kumpokea YESU kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako.

A. imani ni nini?
1: Imani ni kuwa na uhakika wa mambo yanayotarajiwa, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. ebr 11:1.

2: imani ni kuyaona yasiyokuwako kana kwamba yapo. Rumi 4:17.

3:Imani ni kumtegemea MUNGU kwa kila kitu. mith 3:5-6.

4: imani ni kusadiki ya kwamba kila alichokisema MUNGU atakifanya. Rumi 4:19.

Kwa leo tuishie hapa ni imani yangu kuwa umepokea kitu kupitia somo hili. naomba tukutane tena katika sehemu inayofuata
 ITAENDELEA.

No comments:

Post a Comment