Sehemu ya pili.
B: MSIGI WA IMANI.
Warumi10:17.Basi imani chanzo chake ni kusimkia na kusikia, na kusikia huja kwa neno la kristo.
Good news Bible inasema, hivyo basi imani inatokana na kusikia ujumbe, na huo ujumbe unatokana na neno la Kristo.
Msingi maana yake mahali ambapo kitu kinaanzia au mwanzo wa kitu. Kwa hiyo imani yoyote iliyo nje ya neno la Kristo hiyo sio imani sahihi, na imani hiyo haiwezi kuleta muujiza unaotarajia kutoka kwa Mungu. Kwa hiyo kulisikia neno la Kristo kunazaa imani na hiyo imani inazaa haki na hiyo haki inazaa muujiza wako. Lakini pia watu wengi wamesikia neno la Mungu na kuliamini lakini halijazaa matunda kwenye maisha yao. unafikiri ni kwa nini? soma andiko lifuatalo Yak.2:14-17 - ndugu zangu yafaa nini mtu akisema anayo imani lakini hana matendo? je! ile imani yaweza kumuokoa? hapa ndipo watu wengi hukwama. Umesikia neno na kuliamini usikae chini na kuliacha neno lijishughulishe lenyewe. Baada ya kusikia neno la Kristo na kuliamini chukua hatua ya kufanya matendo ya imani. kwa mfano wewe ni mlemavu na neno la MUNGU likaja kwako kwamba ni wakati wa MUNGU sasa kukuondoa katika hali uliyonayo, kama utaendelea kukaa bila kuchukua hatua ya kunyanyuka pale ulipo sio rahisi kupokea uponyaji. hiyo ndiyo inaitwa matendo ya imani.
Yak. 1:22-24 - Lakini iweni watendaji wa neno wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu wala si mtendaji mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. Maana hujiangalia, kisha huenda zake mara akasahau jinsi alivyo.
Biblia inasisitiza kwamba tusiwe wasikiaji wa neno tu bali tuwe watendaji.
Kumbe kinachoweza kusababisha mabadiliko chanya yatokee katika maisha ya mtu aliyeokoka ni ile imani unapoiingiza kwenye matendo. Au tuseme kwamba kile ulichosikia kutoka kwa Kristo unapaswa ukitende.
Mathayo 7:17, Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili,aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba,mvua zikanyesha, mafariko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile isianguke, maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.
Mtu aliyeweka msingi wa imani yake katika kulisika neno na kulitenda, anafananishwa na mtu mwenye akili, lakini mtu anayeweka msingi wa imani yake katika kusikia tu na wala halitendei kazi anafananishwa na mtu mpumbavu.
Hayo sio maneno yangu, ila ni maneno ya BWANA YESU mwenyewe.
Katika andiko hili BWANA YESU anafundisha kuhusu mambo matatu yanayokuja kuipima imani yako kwamba ni imara kiasi gani.
1: Jambo la kwanza ni mvua inapoanzakunyesha. Anaposema mvua ikanyesha maana yake ni kwamba baraka na mafanikio yakaanza kuonekana. watu wengi wanapokuwa katika hali ngumu kimaisha, wanajitahidi sana kuwa karibu na MUNGU, lakini wakifanikiwa kidogo tu wanarudi nyuma na kuiacha imani. ukimuona mtu wa jinsi hiyo tambua ya kuwa imani ya mtu huyo ilijengwa kwenye mchanga. kumbe mafanikio pia yanaweza kuwa jaribu kwa watu wengine.
2:Jambo la pili ni mafuriko yanapokuja. Mafuriko ni majaribu yanayompata mtu au anapopitia kwenye mambo magumu katika maisha, kama vile, kufiwa, kuvunjika ndoa, kuachishwa kazi, au kushambuliwa na magonjwa mazito, nk. kuna wakati mtu wa MUNGU anaweza kupitishwa katika nyakati ngumu sana katika maisha, unapaswa kusimama na MUNGU usikate tamaa na kurudi nyuma tambua kwamba ni imani yako inapimwa tu, ukiisha kushinda kuna nyakati za furaha sana zinakuja mbele yako. Na ndiyo maana paulo akasema, ni nini kitanitenga na upendo wa KRISTO paulo hakuona cha kumtenga na upendoKRISTO wa nami nikutie moyo ya kwamba kamwe usikubari kuiacha imani kwa sababu ya magumu unayopitia. SONGA MBELE.
3:Jambo la tatu ni pepo zinapoanza kuvuma. Pepo zinapoanza kuvuma ni ushindani mkubwa unaoendelea sasa katika huduma, ashukuriwe MUNGU wa mbinguni kwa kuendelea kuinua huduma mpya na zenye nguvu sana kila inapoitwa leo. jambo hilo ni jema sana kwa ujumla wake, ila, kuna watu ambao kuinuka kwa huduma nyingi kumewafanya kuchanganyikiwa badala ya kuwa baraka kwao. Ni watu ambao kuongezeka kwa huduma kumewafanya kuwa wazurulaji, hawana kituo wala hawana baba wa kiroho, wao ni waumini wa huduma mpya. watu hawa ni rahisi kuanguka na kurudi nyuma kwa sababu hawana muda kujifunza neno la MUNGU na hivyo wanakuwa wamekosa mizizi ya imani.

No comments:
Post a Comment