Popular Posts

Sunday, 28 June 2015

SOMO: IMANI




Sehemu ya nne





HATUA TATU ZA IMANI



Ili imani ilete matokeo katika maisha yako inakupasa kupita katika hatua  tatu kama ifuatavyo.



1: KUWA NA LENGO LILIO WAZI,


Hatua hii ya imani inakuja mara baada ya mtu kulijaza neno kwa wingi ndani yake.
Unapolisoma neno la MUNGU au kulisikia ,kuna kweli fulani unazikuta mle ndani ya neno, na kweli  hizo zitaleta  msukumo ndani yako wa kutaka kulitendea kazi neno la MUNGU

Hatua hii ndio humpelekea mtu kufanya maamuzi magumu ya kiimani na maamuzi hayo ndiyo yanayoweza kuleta mabadliko makubwa katika maisha yake.

LK 15:17-19. Alipozingatia moyo mwake, akasema, ni watumishi wangapi wa baba yangu wanakula chakula na kusaza,namimi hapa nakufa na njaa. Nitaondoka nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sisitahiri kuitwa mwana wako tena; nifanye kuwa mmoja wa watumwa wako.

Habari hii inamhusu mwana mpotevu, tunaona hapa kwamba baada ya kuteseka sana kijana huyu alipata ufahamu moyoni mwake, baba yake anamiliki kila kitu halafu yeye anakula na nguruweakafanya uamuzi.
Uamuzi alioufanya ni kurudi kwa baba yake na kutubu, aliamini moyoni mwake atakapo chukua hatua hiyo ya kutubu baba yake atamsamehe na hatakufa na njaa tena. Na uamuzi huo ulileta mabadiriko makubwa sana katika maisha yake.
Imani inakaa ndani ya moyo wa mtu, na ukiicha ndani yako tu, haitaleta mabadiriko yoyote ndani yako na badala yake hata imani yenyewe itaishia kufa.
Soma neno la MUNGU na uliamini kisha chukua uamzi wa kulitendea kazi ndipo utayaona matunda ya imani yako.

2: KUTAMKA HADHARANI KUHUSU KILE UNACHOKIAMINI  [ukiri]

MK 5:27-28. Aliposikia habari za YESU alipita katika  mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake. Maana  alisema nikiyagusa mavazi yake tu nitapona. Mara chemichemi ya damu yake yake ikakauka, naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba wake ule.

Mwanamke huyu alifanya uamuzi mgumu,  Kwa mila za wayahudi mwanamke mwenye tatizo kama hilo alikuwa ni najisi na hakuruhusiwa kukaa katikakati ya watu wengine.
Kwa hiyo alichokuwa anafanya pale ni jambo ambalo lingeweza hata kumsabababishia kifo.
Wanathiolojia wanasema mwanamke huyu alikuwa anatamka maneno haya kwa kurudia rudia mara nyingi. nikiyagusa mavazi tu nitapona
Hatua hii ya kutamka ni mhimu sana kwenye safari hatua ya kupokea majibu yake.

Kumbuka kuna nguvu kubwa iliyojificha nyuma ya maneno yako, kushinda kwako au kushindwa kwako kwa kiasi kikubwa kumechangiwa na maneno yako. 

MWa 1;1-3 inasema, Hapo mwanzo MUNGU aliziumba mbingu na nchi, nayo nchi ilikuwa ukiwa tena utupu, na giza lilikuwa juu ya vilindi vya uso wa maji, Roho ya MUNGU ikatulia juu ya uso wa maji MUNGU akasema iwe nuru ikawa nuru 
Maandiko ya yanaonyesha jinsi ambavyo MUNGU aliumba mbingu na nchi  kwa kutamka maneno tu, hii ina dhihirisha kuna nguvu katika kutamka.
Biblia inasema Roho ya MUNGU ilipotulia juu ya uso wa maji ndipo alisema iwe nuru na ikawa. Sasa basi kwa wewe uliteokoka ndani yako kuna nguvu ile ile iliyokuwa imetulia juu ya uso wa maji.
Sasa, unapotamka na kukiri vitu dhaifu hivyo ndivyo vinavyoweza kutokea katika maisha yako.

Ninchotaka ujue hapa nikwamba kama umemwamini katika jambo fulani, hakikisha una likiri jambo hilo mara kwa mara mbele za MUNGU na wakati mwingi unaweza kukiri hata kwa watu wengine, na kwa kadiri unavyo endelea kukiri na kulitamka mara kwa mara ndivyo jambo hilo litaumbika kwenye ulimwengu wa roho na kutokea kwenye ulimwengu huu.

Mith 18:21 inasema, Uzima na mauti huwa katika uwezo wa ulimi, nao wao waupendao watakula matunda yake. 
Tamka mambo yanayohusu uzima ili upate kuishi na sio mauti, tamka baraka na sio laana. ndipoutamuona MUNGU.

Kum 30:30, Lakini neno hili li karibu nawe sana, li katika kinywa chako na moyo wako upate kulifanya.
Kama unataka kuiona imani yako ikileta mabadiriko makubwa  katika maisha yako jifunze kujitamkia mambo mema.

3:KUATAMIA KILE UNACHO AMINI NA KUKIRI KWA NJIA YA MAOMBI.

Hatua nyingine ya kutembea katika imani ni kukiatamia kwa maombi kile unacho amini na kukikiri.
 Kumbuka, unapotamka juu ya kile unachokiamini unakuwa umetangaza vita na shetani. Namna ya kushinda vipingamizi vyake ni kuatamia kwa njia ya maombi.

1fal 18;41. Katika mistari hii tunaona kwamba Eliya alikuwa ametamka kwamba kuna sauti ya mvua, wakati ambao mvua ilikuwa haijanyesha kwa kipindi cha zaidi miaka  mitatu na nusu.
Baada ya kutamka Eliya alikaa magotini mpaka mvua iliponyesha tena katika nchi ile.
Unapotamka mambo unayotaka yatokee katika maisha yako, usikae tu na kusubiri, mambo yatokee yenyewe, nenda magotini.

 Ukimwani Mungu juu ya jambo lolote mkiri yeye kwamba atafanya, atamia kwa maombi na utauona mkono wa BWANA.

Ni maombi yangu kwa BWANA kwamba akutendee yote unayoamini na kuyakiri katika maisha yako, katika jina la YESU.


 MWISHO



.

Friday, 26 June 2015

SOMO: IMANI



Sehemu ya 3.



Namshukuru sana MUNGU baba wa Bwana wetu YESU kristo aliyetupa uzima na afya njema, nakutuwezesha kuiona tena siku ya leo. pia nikushukuru sana wewe ndugu yangu mpendwa kwa kuendelea kujumuika pamoja nasi katika mfululizo wa masomo haya kutoka katika huduma ya Ruhama healing ministry.wiki iliyopita tulimaliza kwa kuweka msisitizo zaidi kaatika kulisoma na kulitendea kazi neno la MUNGU. karibu tuendelee sehemu ya tatu.

AINA TATU ZA NENO.


Tunaposema juu ya kulisikia  na kulitendea kazi neno, tunamaanisha aina tatu za neno, au maeneo matatu ambayo neno la MUNGU hutenda kazi.


1: LOGOS; Ni neno la kiyunani lenye maana ya neno lililoandikwa, au kwa lugha nyingine ni maandiko.Ukweli ni kwamba neno la MUNGU lililoandikwa ndiyo msingi mkuu wa imani.
Hii ni kwa sababu Biblia haikuandikwa kwa mtazamo wa waandishi bali ni kwamba Roho mtakatifu aliwaongoza kuandika yale yote ambayo MUNGU alikuwa amesema nao.  Au tunaweza kusema walivuviwa na Roho mtakatifu kuandika neno la MUNGU. Kwa hiyo hakuna Biblia nyingine itakayoandikwa tena na kuitwa neno la MUNGU.


2: RHEMA. Ni neno la kiyunani lenye maana ya neno lililofunuliwa, Kufunuliwa hapa haina na kupata kitu kipya ambacho hakijawahi kutokea hapana, ni ile hali ya mtu kupata mwanga fulani kwa msaada wa Roho mtakatifu juu ya maana halisi ya kile ambacho MUNGU alimaanisha wakati anatamka maneno hayo,au neno hilo.
Pia inaweza kuwa na maana ya kupata tafsiri halisi juu ya kile kilichoandikwa ndani ya neno la MUNGU kuhusu maisha yako ya sasa au maisha ya mtu mwingine. Ni ukweli wa neno la MUNGU unaowekwa wazi kuhusu maisha yako ya sasa.

3: PROPHETIC WORD: Ni neno la MUNGU linaloletwa kinywani mwa mtu kwa msukumo wa Roho mtakatifu. Neno hili ni tofauti kidogo na neno la kinabii linalotolewa nabii kwa maana ya mtu anayetumika katika ofisi ya kinabii anapokuwa kwenye utendaji wa huduma yake kama nabii. Ni ukiri wa kiimani ambao ni matokeo ya kulijaza neno la MUNGU kwa wingi ndani yako.
Mtu anayelijaza neno laMUNGU kwa wingi kwa maana ya kulisoma na kujifunza, na hasa mtu huyo anpokuwa mwombaji, neno lile halitavumilia kukaa ndani yake, ni lazima litaanza kudai kutoka nje.
Utamkuta mtu huyo akitamka mambo makubwa kwa imani na yanatokea.

Ezekieli 37:4-10. Akaniambia tena, toa unabii juu ya mifupa hii,uiambie enyi mifupa mikavu lisikieni neno la BWANA.Bwana MUNGU aimbia mifupa hii maneno haya,tazama nitatia pumnzi ndani yenu nanyi mtaishi.nami nitatia mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika ngozi, na kutia pumnzi ndani yenu, nanyi mtaishi nanyi mtajua kuwa mimi ndimi BWANA.Basi nikatoa unabii kama nilivyoamriwa, Hata nilpokuwa natoa unabii , palikuwa na mshindo mkuu, natazama tetemeko la nchi,na ile mifupa ikasogeleana mfupa kwa mfupa mwenziwe. Nikatazama kumbe kulikuwa na mishipa juu yake, nyama ikatokea juu yake, ngozi ikafunika juu yake, Lakini haikuwemo pumnzi ndani yake. Ndipo akaniambia, tabiri uutabirie upepo, mwanadamu ukauambie upepo, BWANA MUNGU asema hivi, njoo kutoka pande za pepo nne ,ee pumnzi ukwapuzie hawa waliouawa wapate kuishi. Basi nikatabiri kama alivyoniamuru, pumnzi ikawaingia, wakaishi, wakasimama kwa miguu yao jeshi kubwa mno.

Ingawa muktadha wa habari hii unahusu wana waisraeli na kifo cha kiroho, kuna kitu kingine tunachoweza kujifunza kupitia habari hii. Kitu hicho si kingine ila ni nguvu iliyopo ndani ya ukiri wa neno ambalo MUNGU analitia katika kinywa chako.
Tumeona hapa kwamba MUNGU anamwambia Ezekieli atabiri Ezekieli anatabiri kwa kutamka kila neno ambalo MUNGU analiweka kinywani mwake au kumwamuru, tunaona hapo baada ya Ezekieli kutabibiri mambo makubwa yanatokea.
Mtu aliye na bidii katika kujifunza neno  MUNGU lile neno huwa linahifadhiwa ndani yake, mtu huyu anapokabiliwa na changamoto fulani katika maisha yake, neno huwa lina kawaida ya kuhama kutoka moyoni kuja kinywani, na linapotamkwa kwa upako linakuwa na nguvu ya kubadilisha mazingira yaliyopo na kuwa kama unavyotaka yawe.
Dunia hii na vyote vilivyomo vimeumbwa kwa neno, kwa maana hiyo ni kwamba vina uwezo wa kusikia sauti ya MUNGU kupitia neno na kutii.

Marko 11:23. Amin nawaambia yeyote atakayeuambia mlima huu ng,oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, bali aamini kwamba hayo asemamayo yanatukia, nayo  
yatakuwa yake,
Ndugu yangu mpendwa katika kristo YESU, ni kweli kwamba MUNGU amewaita watu wengi katika huduma ya kinabii,Na ataendelea kufanya hivyo, lakini napenda uje kwamba nabii wa kwanza wamaisha yako ni wewe mwenyewe.
Kuna changamoto nyingine kwenye maisha hazihitaji nabii kutoka mbali aje kuzitatua, Mungu ameweka nguvu yake ya uumbaji ndani yako ili utamke vitu vitokee.

Mithali 18:21. Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi, na wao waupendao watakula matunda yake.
Hali uliyo nayo kwa kiasi kikubwa imechangiwa na yale ambayo umekuwa unatamkia katika maisha yako. Na mara nyingi tumejikuta tunajitamkia mabaya zaidi kuliko tunavyoweza kujitamkia mema. Tubadirike.
ITAENDELEA


Sunday, 21 June 2015

Sarah Maganga akishuhudia jinsi ambavyo Mungu alimtendea muujiza  kwenye biashara. yake
 baada ya maombi.

Mtume David Simbeye akihuburi kanisani RHM

Mtume David Simbeye akiombea watu kanisani

Mtume akimuombea baba ambaye hawezi kuongea vizuri
Mtume akiwaombea watu kanisani

Saturday, 20 June 2015

SOMO: IMANI

Sehemu ya pili.

B: MSIGI WA IMANI.
 

Warumi10:17.Basi imani chanzo chake ni kusimkia na kusikia, na kusikia huja kwa neno la kristo.

Good news Bible inasema, hivyo basi imani inatokana na kusikia ujumbe, na huo ujumbe unatokana na neno la Kristo.
Msingi maana yake mahali ambapo kitu kinaanzia au mwanzo wa kitu. Kwa hiyo imani yoyote iliyo nje ya neno la Kristo hiyo sio imani sahihi, na imani hiyo haiwezi kuleta muujiza unaotarajia kutoka kwa Mungu. Kwa hiyo kulisikia neno la Kristo kunazaa imani na hiyo imani inazaa haki na hiyo haki inazaa muujiza wako. Lakini pia watu wengi wamesikia neno la Mungu na kuliamini lakini halijazaa matunda kwenye maisha yao. unafikiri ni kwa nini? soma andiko lifuatalo Yak.2:14-17 - ndugu zangu yafaa nini mtu akisema anayo imani lakini hana matendo? je! ile imani yaweza kumuokoa? hapa ndipo watu wengi hukwama. Umesikia neno na kuliamini usikae chini na kuliacha neno lijishughulishe lenyewe. Baada ya kusikia neno la Kristo na kuliamini chukua hatua ya kufanya matendo ya imani. kwa mfano wewe ni mlemavu na neno la MUNGU likaja kwako kwamba ni wakati wa MUNGU sasa kukuondoa katika hali uliyonayo, kama utaendelea kukaa bila kuchukua hatua ya kunyanyuka pale ulipo sio rahisi kupokea uponyaji. hiyo ndiyo inaitwa matendo ya imani.

Yak. 1:22-24 - Lakini iweni watendaji wa neno wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu wala si mtendaji mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. Maana hujiangalia, kisha huenda zake mara akasahau jinsi alivyo.

Biblia inasisitiza kwamba tusiwe wasikiaji wa neno tu bali tuwe watendaji.

Kumbe kinachoweza kusababisha mabadiliko chanya yatokee katika maisha ya mtu aliyeokoka ni ile imani unapoiingiza kwenye matendo. Au tuseme kwamba kile ulichosikia kutoka kwa Kristo unapaswa ukitende.
Mathayo 7:17, Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili,aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba,mvua zikanyesha, mafariko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile isianguke, maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.

Mtu aliyeweka msingi wa imani yake katika kulisika neno na kulitenda, anafananishwa na mtu mwenye akili, lakini mtu anayeweka msingi wa imani yake katika kusikia tu na wala halitendei kazi anafananishwa na mtu mpumbavu.
Hayo sio maneno yangu, ila ni maneno ya BWANA YESU mwenyewe.

Katika andiko hili BWANA YESU anafundisha kuhusu mambo matatu yanayokuja kuipima imani yako kwamba ni imara kiasi gani.

1: Jambo la kwanza ni mvua inapoanzakunyesha. Anaposema mvua ikanyesha maana yake ni kwamba baraka na mafanikio yakaanza kuonekana. watu wengi wanapokuwa katika hali ngumu kimaisha, wanajitahidi sana kuwa karibu na MUNGU, lakini wakifanikiwa kidogo tu wanarudi nyuma na kuiacha imani. ukimuona mtu wa jinsi hiyo tambua ya kuwa imani ya mtu huyo ilijengwa kwenye mchanga. kumbe mafanikio pia yanaweza kuwa jaribu kwa watu wengine.

2:Jambo la pili ni mafuriko yanapokuja. Mafuriko ni majaribu yanayompata mtu au anapopitia kwenye mambo magumu katika maisha, kama vile, kufiwa, kuvunjika ndoa, kuachishwa kazi, au kushambuliwa na magonjwa mazito, nk. kuna wakati mtu wa MUNGU  anaweza kupitishwa katika nyakati ngumu sana katika maisha, unapaswa kusimama na MUNGU usikate tamaa na kurudi nyuma tambua kwamba ni imani yako inapimwa tu, ukiisha kushinda kuna nyakati za furaha sana zinakuja mbele yako. Na ndiyo maana paulo akasema, ni nini kitanitenga na upendo wa KRISTO paulo hakuona cha kumtenga na upendoKRISTO wa nami nikutie moyo ya kwamba kamwe usikubari kuiacha imani kwa sababu ya magumu unayopitia. SONGA MBELE.

3:Jambo la tatu ni pepo zinapoanza kuvuma. Pepo zinapoanza kuvuma ni ushindani mkubwa unaoendelea sasa katika huduma, ashukuriwe MUNGU wa mbinguni kwa kuendelea kuinua huduma mpya na zenye nguvu sana kila inapoitwa leo. jambo hilo ni jema sana kwa ujumla wake, ila, kuna watu ambao kuinuka kwa huduma nyingi kumewafanya kuchanganyikiwa badala ya kuwa baraka kwao. Ni watu ambao kuongezeka kwa huduma kumewafanya kuwa wazurulaji, hawana kituo wala hawana baba wa kiroho, wao ni waumini wa huduma mpya. watu hawa ni rahisi kuanguka na kurudi nyuma kwa sababu hawana muda kujifunza neno la MUNGU na hivyo wanakuwa wamekosa mizizi ya imani.



Thursday, 18 June 2015

SOMO; IMANI

Namshukuru sana na MUNGU aliyetupa neema ya kukutana tena katika mfululizo wa masomo haya kutoka katika huduma hii ya Ruhama healing ministry.Nikukaribishe sana katika somo hili ambalo naamini litakuwa ni baraka sana kwako na kwangu pia.

UTANGULIZI.

ANDIKO. EBR 10;30 Biblia inasema. lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani, akisitasita roho yangu haina furaha naye.
Hapa tunaona maandiko yanasema mwenye haki ataishi kwa imani. kwa maana hiyo ni kwamba mwenye haki akiweka imani pembeni hataweza kuishi.
Au niseme kwamba imani ndio mtaji mkubwa wa kumwezesha mwenye haki kuishi hapa duniani.
Mwenye haki ni mtu aliyempokea YESU kuwa BWANA na mwokozi wa maisha yake, na kuishi kwa kufuata maelekezo yake.

Warumi 1:17 Biblia inasema. haki ya MUNGU inadhihirishwa ndani yake{huyo mwenye kuamini}toka imani hadi imani, kama ilivyoandikwa, mwenye haki ataishi kwa imani.
kumbe kinachomfanya mtu kuwa mwenye haki mbele za MUNGU ni imani iliyomo ndani yake na si vinginevyo.
Na si imani iliyomo ndani yake tu bali imani inayokuwa  kutoka kiwango fulani kwenda kwenye kiwango kingine.
Na kwa kadiri viwango vyako vya imani vinavyoendelea kukua na kuongezeka, ndivyo haki yako mbele za MUNGU inavyokua na kuongezeka.
Kuongezeka kwa haki yako mbele za MUNGU kuna harakisha mabadiliko katika maisha yako, ya kiroho na kimwili.
Wagaratia3:11 inasema. Ni dhahiri kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za MUNGU katika sheria, kwa sababu mwenye haki ataishi kwa imani.
Maandiko haya yote yanaongelea kitu kilekile, kwamba mwenye haki ataishi kwa imani hapa tunapata picha moja tu, kwamba imani ndiyo injini ya kuyasukuma maisha yake na kuyafanya yasonge mbele.
Kwa maana iliyowazi zaidi ya maandiko hayo ni kwamba kama huna imani unapoteza haki yako ya kupokea chochote kutoka kwa MUNGU.
Waebrania 11:6 lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza,kwa maana mtu amwendeaye MUNGU lazima aamini kwamba yeye yuko, na huwapa thawabu wamtafutao.
Hapa inaendelea kutafsiri kwa undani zaidi, kwamba pasipo imani haiwezekani kumpendeza MUNGU, rugha nyepesi ya neno hili ni kwamba kutokuwa na imani ni dhambi.
 Unaweza kuona ni kwa jinsi gani imani ni mhimu katika maisha ya mtu aliyeokoka,  hata wale watakaoenda jehanamu, hawataenda kwa sababu wametenda dhambi sana, ila wataenda jehanamu kwa sababu ya dhambi kubwa kupita zote, nayo ni kukata kumwamini YESU.
kama kuna mtu unafuatilia mafundisho haya na unajua kuwa hujaokoka, huu ndio wakati mwafaka wa kumpokea YESU kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako.

A. imani ni nini?
1: Imani ni kuwa na uhakika wa mambo yanayotarajiwa, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. ebr 11:1.

2: imani ni kuyaona yasiyokuwako kana kwamba yapo. Rumi 4:17.

3:Imani ni kumtegemea MUNGU kwa kila kitu. mith 3:5-6.

4: imani ni kusadiki ya kwamba kila alichokisema MUNGU atakifanya. Rumi 4:19.

Kwa leo tuishie hapa ni imani yangu kuwa umepokea kitu kupitia somo hili. naomba tukutane tena katika sehemu inayofuata
 ITAENDELEA.

Friday, 12 June 2015

Mtume David Simbeye akisisititiza katika moja ya ibada zinazofanyika katika huduma ya Ruhama healing ministry iliyoko Tabata kisukuru jijini Dar es salam. Mungu amekuwa akimtumia sana mtume David Simbeye katika kuwafungua watu waliofungwa kwenye vifungo mbailmbali, katika ibada hizo zinazofanyika kila siku za kanisani hapo.

Friday, 5 June 2015

KUTOKA GIZANI KUINGIA NURUNI

Ndugu mpendwa wangu wewe ambaye umekuwa ukifuatilia mafundisho yetu kutoka ktk huduma hii. napenda kukushuru sana kwa kuwa miongoni mwa maelfu ya watu wanaoungana nasi huduma hii. Pia napenda pia napenda kuwaomba radhi wote kwa kuto kupost masomo yetu kwa muda kidogo. hii ni kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu. karibu tujumuike pamoja kwenye hili jipya ambalo naamini litakuwa baraka sana kwako.



Andiko; Isaya 2;5 Biblia inasema. Enyi wa nyumba ya israeli njoni twende ktk nuru ya BWANA.
Hapa tunaona nabii akiwa himiza wana wairaeli waje kwenye nuru ya BWANA.


Wakati nabii anasema maneno haya wana waisraeli wakati huo walikuwa wako kwenye nchi kaanani nchi ambayo MUNGU alikuwa amewaambia habari zake kuwa ni nchi iliyojaa maziwa na asali.

Kwa hiyo MUNGU anapowaambia waje kwenye nuru maana yake ni kwamba walikuwa gizani ingawa tayari walikuwa wameshaingia kwenye nchi ya ahadi.


kwa rugha ya sasa hivi tunaweza kusema, pamoja na kwamba walikuwa wameokoka walijikuta wanaishi au kutembea gizani.


Kutembea gizani kuna weza kuwa na maana ya; kuishi maisha yasiyokuwa na matumaini juu ya maisha yao yao ya baadae. ni maisha ambayo kila kitu kinakuwa kimekwama.
Au niseme kwamba umeokoka vizuri kabisa lakini zile ahadi za MUNGU kwa watu wake huzioni kabisa katika maisha yako. ingawa unaona ndugu zako katika KRISTO wanafanikiwa nawanakuja na shuhuda nzitonzito lakini kwako hakuna kinachotokea, usikate tamaa ndiyo MUNGU amenipa ujumbe huu niulete kwako. Sikiliza, kuna vitu vilivyo sababisha wana waisraeli waishi gizani huku wakiwa kwenye nchi ya ahadi.
Unaposoma neno la MUNGU katika. Kumbukumbu la tolati 18; 9-12 utaona ya kwamba MUNGU alikuwa amemewaambia wana waisraeli wajiepushe na mambo maovu ya kishirikina ambayo wenyeji wa nchi ile walikuwa wanayafanya, mambo ambayo ndiyo yaliyo sababisha MUNGU awatimue kwenye nchi ilena kuwapa wana waisraeli.
Ajabu ni kwamba wana waisraeli walipoingia kwenye nchi ile walisahau maagizo hayo na kuanza kuwaiga wenyeji, jambo ambalo lilisababisha giza litawale katika maisha yao.
Kwa  kifupi ni kwamba mtu aliyeokoka hawezi kutembea gizani kuwepo kitu kinachosababisha hali hiyo.
SWALI; Ni sababu zipi zinazo sababisha mtu aliyeokoka kutembea gizani?



SABABU TATU ZINAZO SABABISHA MTU ALIYEOKOKA KUTEMBEA GIZANI



1. Ni pale tunapovunja mahusiano yetu na MUNGU kwa kutenda dhambi.
isaya 59;1-2 inasema. tazama mkono wa BWANA haukupunguka hata nisiweze kuokoa.wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha na Munguwenu.na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kuskia.
Ndugu yangu mpendwa, dhambi ndiyo chanzo kikubwa au nyezo kubwa ambayo shetani huitumia kaharibu maisha ya watu. kosa moja tu la Adamu limepelekea dunia nzima kutembea gizani, kumbuka shetani anawinda maisha yako kila siku akiipata fursa hujua sana namna ya kuitumia.
Kwa hiyo nichukue nafasi hii kukushauri kwamba endapo unaona unafanya vitu haviendi hebu rudi uangalie kwa upya uhusiano wako na MUNGU ukoje.


2; Ni mashambulizi kutoka kwenye madhabahu iliyo na uhusiano nawewe.


kutoka 20; 4-5 usijifanyie sanamu ya kuchonga wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni; wala kilicho chini duniani ,wala kilicho majini chini ya dunia usijudie wala kuvitumikia kwa kuwa mimi BWANA MUNGU weko niMUNGU mwenye wivu nawapatitiliza wana uovu wa baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfuelfu wanipendao na kuzishika amri zangu.
Unapochunguza na kuona hakuna dhambi katika maisha yako ambayo haijatubiwa, lakini unatembea gizani, chunguza kwenye ukoo wako inawezekana kuna madhabahu iliyojengwa huko nyuma, na pengine hata sasa kuna watu kwenye ukoo wako wanaendeleza ibada hizo, na jina lako likihusishwa. kinachotekea ni kwamba mashetani yanayoabudiwa kwenye madhabahu ile ndiyo yanakuja kukushambulia.
madhabahu za shetani ni kama vile. mahali wanapofanyia matambiko, wanapofanyia mikutano ya kichawi, au kama kuna mtu anafanya uganga kwenye ukoo wako. kumbuka jambo hili, usiposhughurika na kuvunja madhabahu hizo, usifikiri shetani naye atanyamaza.



3; Ni mashambulizi kutoka kwenye madhabahu ya miungu iliyoko kwenye eneo unaloishi.


mdo 13;6-12 paulo alikuwa anahubiri injili kwa mtu mmoja aliyekuwa anaitwa sergio. lakini pembeni yake alikuwepo mtu mwingine aliyeitwa bar yesu mchawi.
mchawi huyu ambaye alikuwa ni madhabahu ya shetani inayotembea. kazi aliyokuwa anafanya pale nikumzuia liwali yule asiiamini injili. paulo alipogundua akashughurika na mchawi yule na ndipo injili yake ikafanikiwa.



JINSI YA KUTOKA GIZANI NA KUANZA KUTEMBEA NURUNI



Marko 11;23 inasema. amin nawaambia, yeyote atakayeuambia mlima huu, ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, bali aamini kwamba hayo asemayo yametuki, nayo yatakuwa yake.
 Ninachotaka kuambia hapo ni kwamba uwezo wa kiliondoa giza katika maisha yako uko katika kinywa chako.



HATUA TATU ZA KUKUPITIA KATIKA MAOMBI YA KULIONDOA GIZA KATIKA
MAISHA YAKO.



1; Maombi ya rehema; tubu kwa ajili ya dhambi zako na za ukoo zilizofungua mlango wa nguvu za giza kushambulia maisha giza. mith 28;13



2; vunja madhabahu zote za kiukoo na kifamilia na madhabahu za miungu ya eneo unaloishi.
kumb 12;1-3



3;Jenga madhabahu ya BWANA iliyovunjika na uanze kuliitia jina laBWANA na kutoa sadaka
   1fal 18;30.


Nimatumaini yangu kuwa somo hili limekuwa baraka kwako, naomba tukutane tena katika kipindi kijacho,
kwa maombi na ushauri wasiliana nasi kwa namba zifuatazo. +255758 928295, +255715928295