Ndugu yangu mpendwa, namshukuru sana MUNGU wangu kwa kutuoa nafasi nyingi ya kuiona siku ya leo. karibu kwenye mfululizo wa masomo haya kutoka katika huduma hii ya Ruhama healing ministry. leo tunakuletea somo jingine lenye kichwa kinachohusu IMANI.
UTANGULIZI:
ANDIKO: EBR 10:38 Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani ,Naye akisitasita ,roho yangu haina furaha naye.
Mwenye ni mtu aliye mpokea YESU kama BWANA na mwokozi wa maisha yake.
Mwenye haki hataishi kwa sababu ya wingi wa vitu alivyo navyo bali ataishi kwa imani.
Imani ndiyo mtaji wakumuwezasha mtu wa MUNGU kuishi hapa duniani.
warumi 1:17 Haki ya MUNGU inadhihirishwa ndani yake, toka imani hadi kama ilivyoandikwa, mwenye haki wangu ataishi kwa imani.
Kumbe kinachomfanya mtu mwenye haki ni imani iliyomo ndani yake. kwa maana hiyo ni kwamba kama hauna imani unapoteza haki ya kupokekea chochote kutoka kwa MUNGU .
lakini pia MUNGU anapenda kuona imani yako ikikua kutoka imani hadi imani.
Galatia 3:11 Ni dhahiri kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za MUNGU katika sheria, kwa sababu mwenye haki wangu ataishi kwa imani.
Wakati wa agano la kale watu waliishi kwa kuifuata sheria, wakati wa agano jipya hatuishi tena kwa sheria, bali tunaishi kwa imani.
Ebr 11:6 lakini paspo imani haiwezekani kumpendeza kwa maana kila mtu amwendeae lazima aamini kwamba yeye yuko na huwapa thawabu wamtafutao.
Andiko hili linaongea kwa uwazi zaidi. Kwa lugha nyepesi ya andiko hilo tunaweza kusema kwamba kutokuwa na imani ni dhambi.
kumbe kuna vitu vingi tunavikosa katika maisha yetu si kwa sababu ya dhambi nyingine yeyete ile bali ni kwa sababu ya dhambi hii ya kukosa imani.
A.
No comments:
Post a Comment