Sehemu ya nne
HATUA TATU ZA IMANI
Ili imani yako iweze kuleta matokeo katika maisha yako, unapaswa kupita katika hatua tatu kama ifuatavyo.
1: Kuwa na lengo lililo wazi
Hatua hii inakuja baada ya mtu kulijaza neno la MUNGU ndani ya mtu. Kumbuka jambo hili, msingi wa imani ni neno la kristo. Kwa hiyo, unapolijaza neno la MUNGU kwa wingi ndani yako hapo ndipo imani huzaliwa, na imani ikizaliwa, imani hiyo itaanza kuleta msukumo ndani yako wa kuliingiza neno hilo ulilojifunza kwenye matendo.
Au niseme hivi, unapolisoma au kulisika neno la MUNGU, kuna kweli fulani utazikuta mle ndani, ambazo zitaleta msukumo wakuliingiza neno hilo kwenye matendo.
Na katika hatua hii, ndipo mtu hufika mahali pa kufanya maamzi ya kiimani, na maamzi hayo yanafanyika ndani ya moyo wa mtu.
Lk 15:17-19. Alipozingatia moyonimwake, alisema,ni watumishi wangapi wa baba yangu, wanaokula chakula na kusaza, na mimi ninakufa na njaa. Nitaondoka na kwenda kwa baba yangu na kumwabia, baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sisitahiri kuitwa mwana wako tena nifanye kuwa mmoja wa watumwa wako.
Habari hii inamhusu mwana mpotevu, aliyechukua sehemu ya urithi, na akaitumia kwa anasa na makahaba hatimaye mali yote ikaisha akaanza kuishi maisha magumu sana.
Baada ya mateso hayo kijana huyo alitafakari ni kwa jinsi gani anapata mateso makubwa kiasi kile, wakati baba yake ana kila kitu akapata ufahamu na akchuka uamzi.
Kile kitendo cha kuamua kwamba atarudi kwa baba yake na kuomba msamaha ndicho tunaita kuwa na lengo lililowazi. Na uamzi wake huo ulileta mabadiliko makubwa katika maisha yake..
Mungu. Ni kweli MUNGU ndiye baba yako na ana kila kitu, lakini unaweza kuendelea kuishi maisha uliyo nayo leo mpaka utakapochukua uamzi wa kiimani wa kufanya jambo.
Ni vigumu kutoka kwenye magonjwa yanayokusumbua mpaka utakapojua kwamba uzima na afya ni haki yako.
2:Kutamkaka hadharani kuhusu kile unachokiamini [ukiri]
mk 5:27-28.
No comments:
Post a Comment