
Watu wengi wanadhani MUNGU anafanya upendeleo au ana ratiba maalum kwa ajili ya kubariki lakini sivyo maana maandiko yanasema wazi nijaribuni muone kama sitowabariki Watu wengine wanapokubwa na matatizo wanafikia kumtupia lawama MUNGU mara amewaacha au amesinzia!MUNGU wetu haachi wala kusinzia watu wake wanapokuwa na tatizo ana wasikia na kuwatendea pasipo binadamu kuamua njia ya kupokea muujiza huo.

Kama ilivyo kwa masomo mashuleni kama hesabu na mengine yana kanuni katika kufikia jibu sahihi vilevile MUNGU wetu si wa kuchezewa wala kukumbukwa wakati washida tu, yeye pia ana kanuni zake za kuweza kuzungumza naye,na ili uweze kupokea baraka zako na kuwa na maisha ya mafaniko hapa duniani ni lazima kanuni hizo uzifuate na hapa ndipo utakapoweza kuzifahamu kanuni hizo.

RUAHA HEALING MINISTRY,karibu sana.
No comments:
Post a Comment