Kwenye Biblia popote palipandikwa kazi za shetani kuna maneno mawili yanatumika. Maneno hayo ni;
- Kuzivunja kazi za shetani
- kuziharibu kazi za shetani.
KAZI ZA SHETANI
Kazi za shetani ziko nyingi sana. Na hapa nitaeleza chache kama ifuatavyo;
YOHANA 10:10. Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.
Mstari huu unaonyesha kazi tatu za shetani. Ambazo ni;
- KUIBA
Shetani anatambua kuwa tumebarikiwa kwa baraka zote na tayari ziko kwenye ulimwengu wa roho, na yeye ufanya kuziiba baraka hizo na kusababisha tuishi maisha magumu wakati tumebarikiwa.
2. KUUA
Shetani uua mtu kiroho, akishafanikiwa kumuua kiroho inakuwa ni rahisi kumuua kimwili. Ndiyo maana mtu akianguka dhambini asipotubu mapema anakuwa hatarini kufa kimwili.
3. KUHARIBU
Shetani anaharibu uhusiano wa Mtu na Mungu. Pia Shetani ndiye aletaye uharibifu wa aina zote.
Kazi nyingine za shetani zinaonekana kwenye mistari ifuatayo;
4. KUPOFUSHA FIKRA
2KORINTO 4: 3-4 "Lakini ikiwa injili imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikra zao wasiamini, isiwazukie nuru ya Injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu"
Mtu aliyeokoka ufahamu/ fikra zake uponywa na Roho Mtakatifu. Kuwaza kwake, kufikiri kwake na Kutenda kwake uanza kubadilika. Shetani hamuogopi mtu kwasababu ya Elimu yake, utajiri wake, wala umaarufu wake. Shetani anamuogopoa mtu aliye na Yesu ndani yake, anayeishi kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu, na aliyejaa neno la Mungu ndani yake.
5. KUWAFUNGA WATU KWENYE VIFUNGO MBALIMBALI
LUKA 13:16 "Na huyu mwanamke, aliye uzao wa Ibrahimu, ambaye shetani amemfunga miaka kumi na minne hii, haikumpasa afunguliwe kifungo hiki siku ya sabato?"
Hii ni kazi nyingine ya shetani, shetani uwaweka watu kwenye vifungo mbalimbali. Mwanamke huyu alifungwa na shetani kwa miaka kumi na minne. Watu walikuwa wakimuona amepinda mgongo hawakujua chanzo cha yeye kupinda mgongo. lakini Yesu anasema chanzo cha yule mwanamke kupinda mgongo ni kifungo cha shetani. Baada ya Yesu kukiondoa chazo ile hali ya kupinda mgongo ikaondoka.
BIBLIA inasema nini juu ya kazi za shetani;
1YOHANA 3:8 "Atendaye dhambi ni wa ibilisi; kwa kuwa ibilisi utenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihilishwa ili azivunje kazi za ibilisi"
Kumbe kilichomleta Yesu duniani ni kuzivunja, na kuziharibu kazi za ibilisi. Na muda wote ambao Yesu alifanya kazi hapa duniani misheni yake kubwa ilikuwa ni hiyo. Tunamuona Yesu kwenye huduma yake akiwafungua waliofungwa na mapepo, akiwaponya wagonjwa, akiwatakasa wenye ukoma, kufufua wafu n.k. Hizo ndizo kazi za ibilisi ambazo Yesu alizivunja.
LUKA 10:19 " Tazama nimewapa amri ya kukanyaga nyoka nange, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakacho wadhulu"
Pamoja na kwamba Yesu alizivunja kazi za ibilisi, bado alituachia jukumu la kuiendeleza kazi hiyo. Yesu hayuko hapa duniani kimwili, yeye ni roho na anaishi ndani ya watumishi wake na anaifanya kazi hiyo kupitia watumishi wake.
Somo hili litaendelea juma lijalo.
KWA MAOMBI NA USHAURI:
Wasiliana nasi kwa simu namba;
+255 758 928 295
+255 715 928 295
No comments:
Post a Comment