Popular Posts

Sunday, 24 May 2015

MATUKIO KATIKA PICHA IBADANI RUHAMA HEALING MINISTRY

Waumini wakifuatilia mahubiri Ruhama Healing 

Mtumishi wa MUNGU David Simbeye akiwa katika mahubiri RHM

Akizungumza jambo Mtume Simbeye RHM

Waumini katika umakini mkubwa katika mafundisho hivi karibuni RHM

Kiongozi wa huduma ya Ruhama Rev.David Simbeye akisisitiza jambo katika mahubiri yake hivi karibuni RHM

Wednesday, 6 May 2015

Kwenye Biblia popote palipandikwa kazi za shetani kuna maneno mawili yanatumika.  Maneno hayo ni;
  1. Kuzivunja kazi za shetani
  2. kuziharibu kazi za shetani.
Mungu anatuamuru kuzivunja kazi za shetani kwa sababu tangu Mwanadamu alipokosea shetani amejaza kazi zake kila mahali. Kazi hizi za shetani utazikuta kwenye ndoa, biashara, kazi, huduma, na kila eneo la maisha ya mwanadamu.

KAZI ZA SHETANI
 Kazi za shetani ziko nyingi sana. Na hapa nitaeleza chache kama ifuatavyo;

YOHANA 10:10. Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. 

Mstari huu unaonyesha kazi tatu za shetani. Ambazo ni;
  1. KUIBA
Kazi ya shetani ni kuiba. Shetani yeye uiba haki za msingi za mtu alizopewa na Mungu. Neno la Mungu katika kitabu cha EFESO 1:3  linasema:" Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo"
Shetani anatambua kuwa tumebarikiwa kwa baraka zote na tayari ziko kwenye ulimwengu wa roho, na yeye ufanya kuziiba baraka hizo na kusababisha tuishi maisha magumu wakati tumebarikiwa.

    2.  KUUA
Shetani uua mtu kiroho, akishafanikiwa kumuua kiroho  inakuwa ni rahisi kumuua kimwili. Ndiyo maana mtu akianguka dhambini asipotubu mapema anakuwa hatarini kufa kimwili.

   3. KUHARIBU
Shetani anaharibu uhusiano wa Mtu na Mungu. Pia Shetani ndiye aletaye uharibifu wa aina zote.

Kazi nyingine za shetani zinaonekana kwenye mistari ifuatayo;

   4. KUPOFUSHA FIKRA
 2KORINTO 4: 3-4 "Lakini ikiwa injili imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikra zao wasiamini, isiwazukie nuru ya Injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu"
     Mtu aliyeokoka ufahamu/ fikra zake uponywa na Roho Mtakatifu. Kuwaza kwake, kufikiri kwake na Kutenda kwake uanza kubadilika. Shetani hamuogopi mtu kwasababu ya Elimu yake, utajiri wake, wala umaarufu wake. Shetani anamuogopoa mtu aliye na Yesu ndani yake, anayeishi kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu, na aliyejaa neno la Mungu ndani yake.

   5.  KUWAFUNGA WATU KWENYE VIFUNGO MBALIMBALI
 LUKA 13:16 "Na huyu mwanamke, aliye uzao wa Ibrahimu, ambaye shetani amemfunga miaka kumi na minne hii, haikumpasa afunguliwe kifungo hiki siku ya sabato?"
Hii ni kazi nyingine ya shetani, shetani uwaweka watu kwenye vifungo mbalimbali. Mwanamke huyu alifungwa na shetani kwa miaka kumi na minne. Watu walikuwa wakimuona amepinda mgongo hawakujua chanzo cha yeye kupinda mgongo. lakini Yesu anasema chanzo cha yule mwanamke kupinda mgongo ni kifungo cha shetani. Baada ya Yesu kukiondoa chazo ile hali ya kupinda mgongo ikaondoka.

BIBLIA inasema nini juu ya kazi za shetani;
1YOHANA 3:8 "Atendaye dhambi ni wa ibilisi; kwa kuwa ibilisi utenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihilishwa ili azivunje kazi za ibilisi"

Kumbe kilichomleta Yesu duniani ni kuzivunja, na kuziharibu kazi za ibilisi. Na muda wote ambao Yesu alifanya kazi hapa duniani misheni yake kubwa ilikuwa ni hiyo. Tunamuona Yesu kwenye huduma yake akiwafungua waliofungwa na mapepo, akiwaponya wagonjwa, akiwatakasa wenye ukoma, kufufua wafu n.k. Hizo ndizo kazi za ibilisi ambazo Yesu alizivunja.

LUKA 10:19 " Tazama nimewapa amri ya kukanyaga nyoka nange, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakacho wadhulu"

Pamoja na kwamba Yesu alizivunja kazi za ibilisi, bado alituachia jukumu la kuiendeleza kazi hiyo. Yesu hayuko hapa duniani kimwili, yeye ni roho na anaishi ndani ya watumishi wake na anaifanya kazi hiyo kupitia watumishi wake.

Somo hili litaendelea juma lijalo.

KWA MAOMBI NA USHAURI:

Wasiliana nasi kwa simu namba;

+255 758 928 295
+255 715 928 295

KUZIVUNJA NA KUZIHARIBU KAZI ZA SHETANI

Sunday, 3 May 2015

Ruhama Healing pia haikubaliani na mauaji yanayofanywa kwa ndugu zetu maalibino

Picha za matukio mbalimbali leo katika ibada ya jumapili Ruhama Healing Ministry

kiongozi mkuu wa Huduma ya Ruhama Healing Ministry Mtume David Simbeye akiwa katika mahubiri ya jumapili ya leo tarehe 03 Mei 2015.

Kwaya ya mellinia kutoka kanisa la KKKT Bonyokwa Tabata wakitumbuiza katika ibada iliyofanyika jumapili ya tarehe 03 Mei 2015 katika Hekalu la huduma ya Ruhama Healing Ministry.

 Baadhi ya waumini wa Huduma ya Ruhama healing ministry wakifuatilia mahubiri yaliyokuwa yanatolewa na kiongozi mkuu wa Huduma hiyo Mtume David Simbeye.

Friday, 1 May 2015

Faidi kutazama nyimbo za dini na Uweze kubarikiwa

Mwimbaji wa nyimbo za Injili na mwanahabari kutoka mkoani Manyara nchini Tanzania Faraja Elias Samo katika video yake ya wimbo wa taratibu wa maombi.

MUNGU anatenda kupitia Moyo wako

Watu wengi wanadhani MUNGU anafanya upendeleo au ana ratiba maalum kwa ajili ya kubariki lakini sivyo maana maandiko yanasema wazi nijaribuni muone kama sitowabariki Watu wengine wanapokubwa na matatizo wanafikia kumtupia lawama MUNGU mara amewaacha au amesinzia!MUNGU wetu haachi wala kusinzia watu wake wanapokuwa na tatizo ana wasikia na kuwatendea pasipo binadamu kuamua njia ya kupokea muujiza huo.

Kama ilivyo kwa masomo mashuleni kama hesabu na mengine yana kanuni katika kufikia jibu sahihi vilevile MUNGU wetu si wa kuchezewa wala kukumbukwa wakati washida tu, yeye pia ana kanuni zake za kuweza kuzungumza naye,na ili uweze kupokea baraka zako na kuwa na maisha ya mafaniko hapa duniani ni lazima kanuni hizo uzifuate na hapa ndipo utakapoweza kuzifahamu kanuni hizo.

RUAHA HEALING MINISTRY,karibu sana.