Sehemu ya nne
HATUA TATU ZA IMANI
Ili imani ilete matokeo katika maisha yako inakupasa kupita katika hatua tatu kama ifuatavyo.
1: KUWA NA LENGO LILIO WAZI,
Hatua hii ya imani inakuja mara baada ya mtu kulijaza neno kwa wingi ndani yake.
Unapolisoma neno la MUNGU au kulisikia ,kuna kweli fulani unazikuta mle ndani ya neno, na kweli hizo zitaleta msukumo ndani yako wa kutaka kulitendea kazi neno la MUNGU
Hatua hii ndio humpelekea mtu kufanya maamuzi magumu ya kiimani na maamuzi hayo ndiyo yanayoweza kuleta mabadliko makubwa katika maisha yake.
LK 15:17-19. Alipozingatia moyo mwake, akasema, ni watumishi wangapi wa baba yangu wanakula chakula na kusaza,namimi hapa nakufa na njaa. Nitaondoka nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sisitahiri kuitwa mwana wako tena; nifanye kuwa mmoja wa watumwa wako.
Habari hii inamhusu mwana mpotevu, tunaona hapa kwamba baada ya kuteseka sana kijana huyu alipata ufahamu moyoni mwake, baba yake anamiliki kila kitu halafu yeye anakula na nguruwe , akafanya uamuzi.
Uamuzi alioufanya ni kurudi kwa baba yake na kutubu, aliamini moyoni mwake atakapo chukua hatua hiyo ya kutubu baba yake atamsamehe na hatakufa na njaa tena. Na uamuzi huo ulileta mabadiriko makubwa sana katika maisha yake.
Imani inakaa ndani ya moyo wa mtu, na ukiicha ndani yako tu, haitaleta mabadiriko yoyote ndani yako na badala yake hata imani yenyewe itaishia kufa.
Soma neno la MUNGU na uliamini kisha chukua uamzi wa kulitendea kazi ndipo utayaona matunda ya imani yako.
2: KUTAMKA HADHARANI KUHUSU KILE UNACHOKIAMINI [ukiri]
MK 5:27-28. Aliposikia habari za YESU alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake. Maana alisema nikiyagusa mavazi yake tu nitapona. Mara chemichemi ya damu yake yake ikakauka, naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba wake ule.
Mwanamke huyu alifanya uamuzi mgumu, Kwa mila za wayahudi mwanamke mwenye tatizo kama hilo alikuwa ni najisi na hakuruhusiwa kukaa katikakati ya watu wengine.
Kwa hiyo alichokuwa anafanya pale ni jambo ambalo lingeweza hata kumsabababishia kifo.
Wanathiolojia wanasema mwanamke huyu alikuwa anatamka maneno haya kwa kurudia rudia mara nyingi. nikiyagusa mavazi tu nitapona
Hatua hii ya kutamka ni mhimu sana kwenye safari hatua ya kupokea majibu yake.
Kumbuka kuna nguvu kubwa iliyojificha nyuma ya maneno yako, kushinda kwako au kushindwa kwako kwa kiasi kikubwa kumechangiwa na maneno yako.
MWa 1;1-3 inasema, Hapo mwanzo MUNGU aliziumba mbingu na nchi, nayo nchi ilikuwa ukiwa tena utupu, na giza lilikuwa juu ya vilindi vya uso wa maji, Roho ya MUNGU ikatulia juu ya uso wa maji MUNGU akasema iwe nuru ikawa nuru
Maandiko ya yanaonyesha jinsi ambavyo MUNGU aliumba mbingu na nchi kwa kutamka maneno tu, hii ina dhihirisha kuna nguvu katika kutamka.
Biblia inasema Roho ya MUNGU ilipotulia juu ya uso wa maji ndipo alisema iwe nuru na ikawa. Sasa basi kwa wewe uliteokoka ndani yako kuna nguvu ile ile iliyokuwa imetulia juu ya uso wa maji.
Sasa, unapotamka na kukiri vitu dhaifu hivyo ndivyo vinavyoweza kutokea katika maisha yako.
Ninchotaka ujue hapa nikwamba kama umemwamini katika jambo fulani, hakikisha una likiri jambo hilo mara kwa mara mbele za MUNGU na wakati mwingi unaweza kukiri hata kwa watu wengine, na kwa kadiri unavyo endelea kukiri na kulitamka mara kwa mara ndivyo jambo hilo litaumbika kwenye ulimwengu wa roho na kutokea kwenye ulimwengu huu.
Mith 18:21 inasema, Uzima na mauti huwa katika uwezo wa ulimi, nao wao waupendao watakula matunda yake.
Tamka mambo yanayohusu uzima ili upate kuishi na sio mauti, tamka baraka na sio laana. ndipoutamuona MUNGU.
Kum 30:30, Lakini neno hili li karibu nawe sana, li katika kinywa chako na moyo wako upate kulifanya.
Kama unataka kuiona imani yako ikileta mabadiriko makubwa katika maisha yako jifunze kujitamkia mambo mema.
3:KUATAMIA KILE UNACHO AMINI NA KUKIRI KWA NJIA YA MAOMBI.
Hatua nyingine ya kutembea katika imani ni kukiatamia kwa maombi kile unacho amini na kukikiri.
Kumbuka, unapotamka juu ya kile unachokiamini unakuwa umetangaza vita na shetani. Namna ya kushinda vipingamizi vyake ni kuatamia kwa njia ya maombi.
1fal 18;41. Katika mistari hii tunaona kwamba Eliya alikuwa ametamka kwamba kuna sauti ya mvua, wakati ambao mvua ilikuwa haijanyesha kwa kipindi cha zaidi miaka mitatu na nusu.
Baada ya kutamka Eliya alikaa magotini mpaka mvua iliponyesha tena katika nchi ile.
Unapotamka mambo unayotaka yatokee katika maisha yako, usikae tu na kusubiri, mambo yatokee yenyewe, nenda magotini.
Ukimwani Mungu juu ya jambo lolote mkiri yeye kwamba atafanya, atamia kwa maombi na utauona mkono wa BWANA.
Ni maombi yangu kwa BWANA kwamba akutendee yote unayoamini na kuyakiri katika maisha yako, katika jina la YESU.
MWISHO
.