Popular Posts

Saturday, 1 August 2015

SOMO; UTOAJI WA ZAKA



Utoaji wa zaka ni moja kati ya maagizo ya Mungu kwa watu wake wanayopaswa kuyafanya.
Tofauti na sadaka nyingine zaka sio sadaka ambayo wewe unaweza kuchagua ni kiasi gani utoe kwa maneno mengine ni kwamba sadaka ya zaka ni lazima na sio ombi.

kama ilivyo kwa sadaka nyingine kuna baraka nyingi zinazoambana na utoaji wa zaka, kama tutakavyoona huko mbele.

Mwanzo 2:16-17 Biblia inasema, Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu akisema,matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo hakika utakufa

Tunaona hapa kwamba Mungu kabla hajamuumba mwanadamu alitangulia kumtengenezea mazingira mazuri ya kuishi.Mungu alihakikisha kila atakachokihitaji Adamu anakikuta pale bustanini.
Hiyo inaonyesha kwamba mwanadamu ameumbwa na asili ya utajiri.

Kwa hiyo katika utajiri huo ambao Mungu alimpa Adamu Mungu alimruhusu kula matunda yote isipokuwa matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
Kwanini Mungu amruhusu Adamu kula matunda mengine yote kasoro matunda ya mti mmoja tu?
Ni kwamba matunda yale yalikuwa kipimo cha utii wake kwa Mungu, ina maana kila wakati Adamu alipokuwa akipita bustanini akiona mti ule alikuwa anakumbushwa kumtii yeye aliya muumba na kumpa vitu vyote.

Kupitia jambo hilo tunajifunza kwamba umepewa vitu vyote na Mungu kuwa urithi wako, lakini katika vitu hivyo kuna sehemu  ya vitu hivyo ambayo Mungu hajakuruhusu kuvitumia nayo ni zaka.
Kumbuka jambo hili, kwamba katika kila kitu alichokupa Mungu ndani ya vitu hivyo kuna kitu ambacho Mungu amekiweka wakfu kwa ajili yake.
Kilichomfanya Adamu aadhibiwe siyo tunda bali ni lile agizo alilopewa na Mungu kwamba asile matunda ya mti ule. kwa maana nyingine ni kwamba kama Mungu asingekuwa amemkataza kula matunda yale angekula na asingepata madhara yoyote.

Mwa 14:18-20 Na Melkizedeki mfalme wa salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu aliye juu sana. akambariki akisema Abrahamu na abarikiwe na Mungu aliye juu sana. muumba wa mbingu na nchi. Ahimidiwe Mungu aliye juu sana aliye watia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.

Zaka ni sehemu ya kumi ya mapato yako vyote, fedha, mazao, mifungo nk. 
Utoaji wa fungu la kumi haujaanza leo, tunaona hapa kwamba utoaji wa fungu la kumi ulianza tangu wakati wa Ibrahimu. na inawezekana Abraham naye aliwakuta waliomtangulia wanatoa zaka naye akjifunza kutoka kwao. 
Tunaona hapa kwamba abrahamu ametoka kupigana vita, akiwa ameteka nyala nyingi sana. kisha tunaona anakutana na kuhani wa Mungu aliye juu sana na anampa kuhani sehemu ya kumi ya nyala zake. 
Tunajifunza nini hasa juu ya habari hii? Tunajifunza kwamba kila unapotoka nyumbani kwako asubuhi kwenda kazini, kwenye biashara, ua shambani unaenda kupigana vita. pasipo Mungu kukurinda unaweza kupatwa na jambo lolote baya, lakini Mungu anakulinda unajikuta umerudi salama bila madhara yoyote, na zaidi ya hapo unatoka ukiwa na nyara nyingi sana, kumbuka Mungu ndiye aliyekuwezesha kupata vitu hivyo na kama yeye ndiye aliyekupa unapaswa kumpa sehemu ya kumi ya hizo nyara. 
Lakini pia tunajifunza kwamba kuhani wa Mungu aliye juu ndiye aliyepokea zaka kwa niaba ya Mungu, kwa hiyo anayepaswa kupokea zaka kutoka kwako ni kuhani.

Mal 3:7-12 Maandiko haya yanaeleza kwa undani sana kuhusu zaka. Kuna mambo kadhaa tunayoyaona katika mistari hii.

1: kutoa zaka ni agizo la Mungu na kutokutoa zaka ni kurudi nyuma.

Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi nami nitawarudia ninyi. Lakini ninyi mwasema tukurudie kwa namna gani?

Mungu anaposema nirudieni mimi maana yake ni kwamba watu hawa walikuwa mbali nayeye au tuseme walikuwa wamejitenga na Mungu kwa kwa sababu wya kutokutoa zaka. kwa rugha ya leo tungeweza kusema wamerudi nyuma, au wameacha wokovu, hilo sio jambo jepesi.
 
2: Kutokutoa zaka ni kumwibia Mungu au tuseme ni wizi

Aina ya mwizi anayatajwa hapa kwenye biblia ya kiingereza inamfananisha na mwizi wa kutumia silaha.{ will a man rob or defraud god} Kwa hiyo kama mwizi wa kawaida anatumia silaha ili kumpora mtu vitu vyake tena huku anaona ndivyo mwizi wa fungu la kumi anavyomfanyia Mungu.
Je mtu huyu anayempora Mungu kwa namna hiyo atakuwa salama? Mungu atusaidie.

3:Kutokutoa fungu la kumi ni laana

Kumbe ukiacha kutoa fungu la kumi unakuwa umechagua kutembea katika laana.  laana hizi zina kuja kuharibu kila kitu katika maisha yako. Kuna mtu anakuwa amepanga malengo fulani ya kuyatekeleza atakapokuwa amepata pesa. Cha ajabu ni kwamba akipata pesa tu mambo yanaanza kuvurugika, mara mtoto anaumwa akipelekwa hosptalini analazwa kabisa pesa badala ya kwenda kwenye malengo yake inaenda hosptalini, pesa ikiisha mtoto anapona. huo ni utendaji wa laana ya kutokutoa zaka.

4: Kazi ya fungu la kumi ni kufanikisha uwepo wa chakula kwenye nyumbani mwa Mungu

Nyumbani mwa Mungu ni wapi?

Zamani makuhani walikuwa wanaishi hekaluni, nyumba zao zilikuwepo palepale hekalu lilipokuwa. Kandokando ya hekalu pia yalikuwepo maghara ya kuhifadhia vyakula vilivyotolewa sadaka.  mazao hayo yalihifadhiwa pale kwa ajili ya chakula cha makuhani na walawi.

 Kwa kujibu swali hilo ni kwamba nyumbani mwa Mungu ni pale anapopatikana kuhani.

Faida za kutoa fungu la kumi au zaka.

Kwa mjibu wa andiko hilo kuna faida kubwa mbili za kutoa fungu la kumi.

1: Mungu atafungua madirisha yambinguni ili kuachilia baraka zake juu ya maisha yako

2: Mungu atamkemea yule alaye vitu vyako na hasa unapotoa kwa uaminifu

Mungu wangu akubariki sana, na hasa pale utakapoamua kuikata laana na kuchagua baraka kwa kutoa zaka.

Niite mtume David Simbeye kutoka Ruhama healing ministry. kwa maombi na ushauri nipigie kwa namba hii. 0715928295 au 0758928295